Mwimbaji huyo akizungumzia Wanahabari Nandy amesema watu wanamsema ni mjamzito kwa sababu ya ongezeko la mabadiliko yake ya mwili wake ambayo yanasababishwa na ukuaji ila sio ujauzito.
“Watu wanasema mimi ni mjamzito kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wangu ambayo yanasababisha kukua haraka kama kunenepa, ukiangalia familia yetu wote wanamaumbo makubwa halafu ni wanene labda na mimi ndiyo nimefikia hatua ya kuwa hivyo,” amesema Nandy.
Hii si mara ya kwanza kuibuka tetesi kama hizo, Mei mwaka huu ziliibuka tena mara baada ya mabadiliko makubwa katika muonekano wa Nandy zikiwa ni wiki kadhaa kupita tangu wawili hao kuweka wazi ni wapenzi.
Utakumbuka April 10 mwaka huu Rapa Bill Nass alimvisha pete ya uchumba msanii Nandy mara baada ya kusemekana kuwa wapo kwenye mahusiano kwa kipindi kirefu.