Makubaliano hayo yamelenga kuwawezesha abiria wanaosafiri na kuhitaji kuunganisha ndege ili wafike sehemu wanazokwenda
Kupitia makubaliano haya abiria sasa wataweza kusafiri kwa urahisi kati ya Afrika, Doha kwa kuunganisha na mabara ya Asia Pasifiki, Amerika, Ulaya na Mashariki ya Kati
Aidha kwa wasafiri kutoka nje wataweza kusafiri kwa urahisi wakitumia Air Tanzania kwenda Dar, Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Bukoba, Kigoma, Tabora, Mpanda, Mbeya, Songea, Mtwara, Dodoma, Iringa, Bujumbura, Entebbe, Harare, Lusaka, Hahaya.
Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu wa Air Tanzania, Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kuwa makubaliano haya yataongeza wigo wa biashara na kuifanya Air Tanzania kuwa ya ushindani zaidi
Tags
BREAKING NEWS