TAKUKURU Mkoani humo imemkamata Oscar Waluye ambaye ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Olkitikiti kufanya udanganyifu kwenye mitihani ya Darasa la 7 iliyoanza jana.
Anatuhumiwa kuwalazimisha Wanafunzi wawili wa Darasa la 6 kufanya mitihani hiyo badala ya Watahiniwa ambao uwezo wao darasani ni wa kiwango cha chini.
Taasisi hiyo iliwakamata Wanafunzi hao wakiwa tayari wamewafanyia wenzao mitihani ya Kiswahili na Hisabati.
Uchunguzi wa Shauri unaendelea na Mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria pindi utakapokamilika.
Tags
BREAKING NEWS