HARAKATI za malori kati ya Tanzania na Uganda kwenye mpaka wa Mutukula, zimeanza tena baada ya nchi hizo mbili kufi kia makubaliano juu ya hatua za kutekeleza wakati huu wa janga la Covid 19.
Kwa mujibu wa Ofisa Forodha katika mpaka wa Mutukula upande wa Tanzania, William Mkenda, madereva wa malori watatakiwa kupima kama wana maambukizi ya corona kwa mujibu wa miongozo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ya kudhibiti maambukizi mipakani na kukabiliana na usumbufu wa kibiashara.
Mkenda alikuwa akitoa taarifa fupi kwa ujumbe wa Sekretarieti ya EAC, ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Miundombinu na Mipango, Steven Mlote. Ujumbe huo ulikuwa kwenye ziara ya kufanyia tathmini mpaka huo wa Mutukula, ukiwa na lengo la kuangalia maendeleo ya namna Tanzania na Uganda wanatekeleza mpango wa kupunguza misongamano kwenye mipaka.
Kwa mujibu Mkenda, upimaji wa corona katika mpaka huo umelenga kuhakikisha hatari za kiafya zinazohusiana na corona zinapunguzwa. Ujumbe huo wa EAC pia ulikutana na kujadiliana na madereva wa malori katika mpaka huo, kwa lengo la kukusanya changamoto wanazokutana nazo wanapovuka mipaka ya nchi na nchi.
Katika majadiliano hayo, baadhi ya madereva walieleza kutoridhishwa na hali wanayokumbana nayo wakati wa utekelezwaji wa hatua mpya zilizowekwa ili kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo.
Kwa upande wake, Mlote alisema mawaziri na makatibu wakuu wanaohusika na biashara, afya na masuala ya EAC, walifanya mkutano na kuweka miongozo juu ya jinsi madereva wa malori, wanapaswa kuwezeshwa kwenye shughuli zao za kuvuka mipaka. Alisisitiza haja ya watu kuondokana na unyanyapaa katika kushughulikia masuala ya Covid 19.