Dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.9 yataifishwa


Serikali imetaifisha dhahabu ya Kilogram 27.488 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2.9 iliyoingizwa kinyemela kutoka Kenya

Dhahabu hiyo mali ya Mfanyabiashara Bhawesh Chandulal Gandecha, ilikamatwa na Afisa Forodha katika mpaka wa Tanzania na Kenya huko Sirari, May 15, 2020

Meneja wa TRA Mkoa wa Mara, Wallace Mkande, amesema Mfanyabiashara huyo alikamatwa akitaka kuingiza dhahabu hiyo kutoka Kenya kinyemela bila kuwa na nyaraka za kuonesha amelipia ushuru

Mfanyabiashara huyo alipoulizwa alisema ameshalipa ushuru ila hajapewa stakabadhi na kuwa nyaraka nyingine zipo Dodoma huku akipiga simu kwa baadhi ya watu kuwalalamika kwa kushelewesha kuzituma

Alifunguliwa kesi Uhujumu Uchumi katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime na kushtakiwa kwa makosa ya Kuendesha Mtandao wa Uhalifu, Kufanya biashara ya dhahabu bila nyaraka muhimu na kutakatisha fedha

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form