BRAZIL: ZAIDI YA WATU 7,000 WAMEFARIKI NDANI YA WIKI MOJA



Wizara ya Afya nchini humo imeripoti vifo vipya 641, kwa siku ya jana Juni 21, 2020. Hii inaonesha kuwa watu 7,285 wamefariki ndani ya wiki moja

Aidha, nchi hiyo ambayo sasa imerekodi jumla ya vifo 50,617, imerekodi Wagonjwa wapya 17,459 hapo jana na kufanya jumla ya visa kufikia 1,085,038

Kwa takwimu hizo #Brazil ni nchi ya pili kuwa na visa vingi vya #COVID19 duniani huku yenyewe na Marekani zikiwa ndizo nichi zenye visa zaidi ya milioni 1


JUNI 20,2020
BRAZIL YAREKODI VISA ZAIDI YA MILIONI 1


Mlipuko wa Corona unaendelea kushika kasi Amerika ya Kusini na Brazil inakuwa nchi ya pili duniani kurekodi visa zaidi ya Milioni 1

Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 54,771 na kupelekea maambukizi ya nchi hiyo kufikia 1,038,568. Marekani ambayo ni nchi iliyoathitika zaidi na COVID19 ina visa 2,971,346

Aidha, vifo vipya 1,206 pia vimeripotiwa na waliofariki dunia kwa COVID19 nchini humo hadi sasa ni 49,090 huku wagonjwa waliopona wakiwa 520,360

Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO) visa vya Corona vimefikia 9,441,343 duniani, wagonjwa 4,374,705 wamepona na 466,223 wamepoteza maisha

JUNI 17, 2020
BRAZIL: VISA ZAIDI YA 34,000 VYAREKODIWA NDANI YA SAA 24

Wizara ya Afya imeripoti visa vipya 34,918 vya COVID na Brazil ina jumla ya visa 923,834 hadi sasa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya (WHO) wagonjwa 464,774 wamepona

Takwimu hizo zimetolewa wakati Afisa wa juu wa Kikosi kinachoshughulikia ugonjwa huo, Walter Braga Netto akidai mlipuko nchini humo umethibitiwa. Amesema #Brazil inafanya vizuri kuliko mataifa mengi ya Ulaya

Pamoja na ongezeko la maambukizi, vifo vipya 1,282 pia vimerekodiwa ndani ya siku moja na kupelekea idadi ya waliofariki kwa CoronaVirus kufikia 45,456

JUNI 16, 2020
VISA ZAIDI YA MILIONI 8 VYAREKODIWA, WAGONJWA MILIONI 3.9 WAPONA

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) visa 8,717,816 vimerekodiwa ulimwenguni hadi kufikia leo asubuhi. Watu 3,959,884 wamepona na vifo ni 442,387

Ripoti mpya kutoka Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa imesema wenye magonjwa sugu ikiwemo magonjwa ya Moyo na Kisukari wapo hatarini zaidi kufariki kwa COVID-19

Marekani ambayo imeathirika zaidi ina visa 2,785,732, vifo 121,545 huku waliopona wakiwa 842,659. Nchi nyingine ni Brazil (891,556) Urusi (537,210), India (343,026) na Uingereza (296,857)

Barani Afrika, nchi zilizoathirika zaidi ni Afrika Kusini (73,533), Misri (46,289), Nigeria (16,658), Ghana (11,964) na Algeria (11,031)

JUNI 15, 2020
UFARANSA KULEGEZA MASHARTI ZAIDI KUANZIA LEO

Rais Emmanuel Macron amesema masharti yaliyowekwa kudhibiti mlipuko wa COVID19 nchini humo yatalegezwa zaidi kuanzia leo ambapo safari za nchi nyingine za Ulaya zitaruhusiwa

Migahawa na hoteli zitaruhusiwa kuanza kutoa huduma nchi nzima. Mji Mkuu wa Ufaransa, Paris ambao umerekodi idadi kubwa zaidi ya visa nchini humo pia utafunguliwa

Hata hivyo, Rais Macron ameonya kuwa, japo nchi hiyo imepata ushindi wake wa kwanza dhidi ya ugonjwa huo, kuna uwezekano unaweza kurejea tena

Ufaransa ina jumla ya visa 157,223, vifo 29,407 na wagonjwa 72,859 wamepona hadi sasa
   

Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form