WAZIRI AWESO AMALIZA MZIZI WA FITNA KARATU,AAGIZA BEI YA MAJI IWE 1,300 UNITI MOJA.



Waziri wa Maji Jumaa Aweso (MB) ametatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu wilayani Karatu baada ya kuamuru kuwepo kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma ya maji katika Mji huo huku akiagiza bei ya maji inayostahili kutozwa kwa sasa ni sh1,300 kwa uniti1 badala ya sh 3,000.
Aweso ameagiza kuungana kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA) na Mamlaka ya Utoaji wa Huduma ya Maji Vijijini (KAVIWASU) na kutengeneza chombo kimoja ambacho kitatoa huduma kwa wananchi kwa maslahi ya wananchi wa Karatu.


Hatahivyo waziri Aweso ametamka kwamba Rais Samia Hassan Suluhu ameridhia kutoa sh,bilioni 4.5 kwaajili ya mradi mkubwa wa maji wilaya hiyo na kuagiza mamlaka husika zianze kutangaza zabuni ya mkandarasi atakayetekeleza mradi wa kusambaza maji wilayani humo.
Aweso amesema hayo leo baada ya kusikiliza maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa maji wilayani humo ambapo awali kulikuwa na mgawanyiko wa maslahi ikiwemo Kaviwasu kutoza sh, uniti moja kwa sh. 3000 huku Karuwasa ikitoza sh,1,750 kwa bei za majumbani.


Aidha, Amesema uwepo huo wa chombo kimoja kutawezesha maslahi ya wananchi ikiwemo utoaji wa huduma bora za utoaji maji pamoja na kuhakikisha miundombinu ya maji haiharibiki.
Pia Waziri Aweso amesisitiza kuwa hakuna mtumishi yoyote atakayefukuzwa baada ya kuungana Karuwasa na Kaviwasa kwa kuwa watakapoungana lita zaidi ya milioni 6 zitakuwepo ndani ya mamlaka moja ambazo zitakidhi mahitaji ya wakazi wa wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine ameagiza bei atakayotozwa mwananchi wa kawaida kwa hivi sasa iwe ni sh,1,300 kwa uniti 1 wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji( Ewura) ikiendelea kuchakata bei halisi itakayotozwa kwa wananchi juu ya ulipaji wa ankara za maji.


Naye mbunge la jimbo la Karatu, Daniel Awackii amemshukuru Waziri,Aweso kwa kuunganisha bodi hizo mbili na kuwa moja kwaajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa hivi sasa watafanya vikao kwa wanachi kwaajili ya kuwaeleza wananchi kulipa ya bei hiyo ya unit 1,300 kwa kila mmoja badala ya sh,2000 hadi 3000 zinazotozwa na Kaviwasu.


Post a Comment

Please Select Embedded Mode To Show The Comment System.*

Previous Post Next Post

Disqus Shortname

sigma2

Contact Form